Jumatano, 25 Juni 2014

WASHINDI WA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA TANZANIA 2014

WASHINDI WA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA 2014
Tarehe 23 Juni kila mwaka ni siku maalum ya Watumishi wa Umma. Nchi wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) huadhimisha  siku hiyo kwa pamoja kwa lengo la kutambua mchango wa Watumishi wa Umma katika maendeleo ya Nchi zao. Kaulimbiu kwa mwaka 2014 ni “Mkataba wa Misingi na Kanuni za Utumishi wa Umma Barani Afrika ni Chachu ya Kuimarisha Utawala Bora na Uendeshaji wa Shughuli za Serikali kwa Uwazi

Hapa nchini Maadhimisho haya huratibiwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Mwaka 2014 Taasisi za Umma 88 zilishiriki na kushindanishwa katika maeneo mbalimbali ya utoaji huduma.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Y. Sefue alikabidhi zawadi kwa Taasisi zifuatazo zilizofanya vyema zaidi kwa kushiriki katika Maonesho yaliyofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam.

1.     BANDA BORA

(I)                Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
(II)             Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA).
(III)           Wizara ya Maji.

2.     MAPAMBANO DHIDI YA UKIMWI MAHALI PA KAZI

(I)                Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.
(II)             Ofisi ya Rais, Tume ya Utumishi wa Umma.
(III)           Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania.


3.     UBUNIFU KATIKA KUBORESHA UTOAJI HUDUMA

(I)                Wizara ya Maji – washindi kupitia Teknolojia ya kupunguza madini ya floride katika maji kwa kutumia mifupa ya ng’ombe.

(II)             Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)-washindi wa pili kupitia kifaa kiitwacho Umeme tayari “ready Board” kinachowezesha wananchi kupata umeme bila kusuka na kusambaza nyaya za umeme (wiring) katika nyumba.



(III)           Wakala ya Vipimo (WMA)-washindi wa tatu kupitia mfumo wa kieletroniki “Clock in and clock out task information system” unaotumika kudhibiti muda wa kuingia na kutoka kazini.

hongera sana kwa washindi!!!!

Hakuna maoni: