Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-
Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi amestaafu Utumishi wa
Umma.
Akiongea katika hafla fupi
ya makabidhiano ya Ofisi Bw. Yambesi amewashukuru Wakurugenzi na Watumishi wa
Ofisi ya Rais-Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa ushirikiano katika kutekeleza
majukumu na kufikia mafanikio na malengo yaliyopangwa.
“Nimefurahi kufanya kazi na
kila mmoja wenu katika kipindi chote hata pale rasilimali zilipokua chache kila
mmoja wenu alijitahidi kufikia lengo la kuwahudumia wadau wetu” Bw. Yambesi
alisema na kuongeza jambo la msingi ni kuhakikisha Watumishi wanaendelea kujengewa
uwezo ili ubora wa kazi na huduma uendelee kuwa wa kiwango stahili.
Katibu Mkuu Bw. Yambesi
aliainisha kuwa amekua Mtumishi wa Umma kwa muda wa miaka 38 na kwa hilo
anamshukuru Mungu kwa kumwezesha kutekeleza majukumu mbalimbali kwa muda wote aliotumikia
Umma.
Wakati
huohuo, Naibu Katibu Mkuu -Utumishi Bw. HAB Mkwizu alimpongeza Bw.
Yambesi kwa utendaji wake mzuri. “Unastaafu lakini umejenga uwezo kwa wanaobaki
ofisini hivyo kiwango cha huduma zinazotolewa na ofisi na ushirikiano
tutaendeleza” Bw. Mkwizu alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni