OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA
TAHADHARI
Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma inawatahadharisha wananchi wote, ndani
na nje ya nchi kujihadhari na watu wanaotumia jina la Utumishi kuwaibia fedha
na kupoteza muda wao kufuatilia jambo ambalo halipo.
Watu
hao wanatumia majina yafuatayo katika mitandao;
Saving
Foundation Loans na Jakaya Foundation kwa
anuani http://savingfoundation.wapka.mobi/index.xhtml
na kuelekeza kuwa Makao Makuu yapo
kwenye jengo la UTUMISHI.
Namba
za simu zifuatazo zimekuwa zikitumika kuwatapeli wananchi watume fedha; 0715-373307,
0656-037520 na 0762-269376.
Wananchi
epukeni kurubuniwa na watu hao kwani Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma haijishughulishi na kutoa mikopo ya aina yoyote kwa wananchi.
Tangazo
limetolewa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
2
Aprili, 2014
Mawasiliano: permsec@utumishi.go.tz, S.L.P 2483 Dar es Salaam,Simu: + (255) 22 2118531-4
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni