Jumatano, 26 Machi 2014

OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA YAUNGANISHA MIKOA MITATU KATIKA KIKA KAZI

Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma (OR MUU) imeunganisha mikoa mitatu katika kikao kazi kilichoendeshwa kwa njia ya kieletroniki (video conference). kikao hicho kiliwahusisha Makatibu Tawala na Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wa mikoa ya Mbeya, Pwani na Lindi.

Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi alikua mwenyekiti wa kikao hicho ambapo washiriki wa mikoa hiyo mitatu walipewa fursa  ya kuuliza maswali moja kwa moja kwa Watendaji wa OR MUU, na kujibiwa hapo hapo.

Mada nne ziliwasilishwa katika kikao hicho, na zilihusu Utekelzaji wa Mfumo wa OPRAS katika Utumishi wa Umma, Mwenendo wa Utekelezaji wa Masuala ya Anuai za Jamii katika Utumishi wa Umma, na Mafanikio na Changamoto za Utekelezaji wa Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara Serikalini.

Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi wa Rasilimaliwatu w. Emmanuel Mlay (katika picha ndogo) akiwasilisha mada katika kikao hicho.

Hakuna maoni: