Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya
Utumishi wa
Umma Bw. George D. Yambesi akifungua mkutano wa wadau kuhusu Mikataba ya
Utendaji Kazi katika Taasisi za Umma katika hoteli ya Serena jijini Dar es
salaam.
Katibu Mkuu mstaafu Bibi Ruth Mollel akitoa mchango wake wakati wa Mkutano kuhusu
Mikataba ya Utendaji Kazi katika Taasisi za Umma
Katibu mstaafu Tume ya Utumishi Bibi Thecla Shangali akitoa maoni yake kuhusu Mikataba ya Utendaji Kazi katika Taasisi za Umma
Mkutano huo uliandaliwa mahsusi ili wadau waweze
kufahamu mambo muhimu juu ya Mfumo wa Mikataba ya Utendaji Kazi hususan
chimbuko, maana na faida zake, mambo ya
msingi yatakayofanikisha utekelezaji wa mfumo huo, fomu ya mkataba wa
utendaji kazi na vipengele vyake, vigezo vya upimaji wa utendaji kazi wa
taasisi, wahusika wa mikataba na utaratibu wake; utaratibu wa kutoa
taarifa za mikataba ya utendaji kazi,
utaratibu wa kutathmini mikataba ya
utendaji kazi; utaratibu wa kushindanisha Taasisi za Umma; na Taasisi
zinazopendekezwa kuingia katika Mikataba ya Utendaji Kazi .
Sambamba na hilo wadau walipata fursa ya kutoa maoni,
ushauri na mapendekezo juu ya mfumo wa Mikataba ya Utendaji Kazi, na namna bora
ya kuitekeleza katika Taasisi za Umma. Wadau walioshiriki mkutano huo ni pamoja
na watendaji na watendaji wakuu wastaafu katika Taasisi za Umma wakiwemo
Makatibu Wakuu wastaafu, watendaji wakuu wa Asasi za Kiraia (AZAKI),
wanataaluma kutoka vyuo vya Elimu ya juu, wawakilishi kutoka katika sekta
binafsi na Washauri waelekezi Wanaojitegemea.
Sehemu
ya baadhi ya wadau walioalikwa katika Mkutano kuhusu Mikataba ya
Utendaji Kazi katika Taasisi za Umma wakimsikiliza mgeni rasmi Katibu
Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D.
Yambesi (hayupo pichani)
Wadau walioshiriki mkutano kuhusu Mikataba ya Utendaji Kazi katika Taasisi za Umma wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. George D. Yambesi (wa sita kutoka kulia mstari wa mbele), kulia kwake ni Naibu Katibu Mkuu Bw. HAB Mkwizu na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri Kazi Bw. Mick KilibaKatibu Mkuu mstaafu Bibi Ruth Mollel akitoa mchango wake wakati wa Mkutano kuhusu
Mikataba ya Utendaji Kazi katika Taasisi za Umma
Katibu mstaafu Tume ya Utumishi Bibi Thecla Shangali akitoa maoni yake kuhusu Mikataba ya Utendaji Kazi katika Taasisi za Umma
Wadau
wakiwasilisha maoni na mapendekezo baada ya kufanya kazi ya vikundi kuhusu Mikataba ya
Utendaji Kazi katika Taasisi za Umma
Mdau kutoka AZAKI ya FORDIA akitoa mchango wake kuhusu Mikataba ya Utendaji Kazi katika Taasisi za Umma
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu akifunga mkutano wa wadau kuhusu Mikataba ya Utendaji Kazi katika Taasisi za Umma uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni