Ijumaa, 22 Novemba 2013

OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA YAFANIKISHA MKUTANO KAZI KWA NJIA YA MTANDAO "VIDEO CONFERENCE"

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu akifungua kikao kazi kwa njia ya mtandao "Video Conference" kilichowakutanisha watendaji kutoka mikoa ya Mara, Rukwa, Ruvuma na Shinyanga
Mkutano kazi kwa njia ya Mtandao ukiendelea: Sehemu ya washiriki wa mkutano kama wanavyoonekana katika kioo cha Runinga "Screen", picha kubwa ni Mkoa wa Ruvuma na picha ndogo ni mikoa ya Mara, Ruvuma, na Shinyanga  ambapo mawasiliano ni ya moja kwa moja, ikijumuisha picha na sauti.

  Mmoja wa washiriki wa mkutano kazi baina ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na watenda kutoka mikoa ya Rukwa, Ruvuma, Mara na Shinyanga akiuliza swali. Picha ndogo kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu akisikiliza maswali.


Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma imeendesha mkutano kazi kwa njia ya mtandao "Video Conference" na Wakurugenzi wa mamlaka za Serikali za Mitaa wa Mikoa ya Mara, Rukwa, Ruvuma na Shinyanga kama taswira hapo juu zinavyoonesha.
Mkutano huo umewakutanisha kwa pamoja watendaji hao moja kwa moja wakiwa katika ofisi zao bila kuingia gharama za kusafiri nje ya vituo vyao vya kazi, hivyo kuokoa rasilimali fedha na muda ili kutoa huduma kwa wananchi.

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu amesema mikutano hiyo itaendelea kwa mikoa yote hapa nchini kushirikishwa, ambapo watendaji kutoka mikoa hiyo watapata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali wanayokabilina nayo katika utendaji kazi katika Utumishi wa Umma.

Teknolojia hiyo ya kisasa kwa mara ya kwanza ilitumika kuwakutanisha watendaji kutoka mikoa ya Kilimanjaro, Kagera na Iringa.

Hakuna maoni: