Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mhe. Celina O. Kombani (Mb) akiongea katika hafla fupi aliyoiandaa ofisini kwake kuipongeza timu ya mpira wa Pete kwa kunyakua ubingwa wa mpira wa Pete katika mashindano ya mei Mosi 2014. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAB Mkwizu.
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Bw. HAb Mkwizu akichukua wasaa wa kuipongeza timu hiyo , kuwashauri Watumishi kushiriki katika michezo mingi zaidi. Aidha alisema kuandaa Bonanza mara moja kila mwezi ni muhimu ili kupata vikosi imara katika michezo mbalimbali.
Kapteni wa Timu ya Utumishi Elizabeth Fussi akimkabidhi Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Mh. Celina O. Kombani kombe la ubingwa waliounyakua katika mashindano ya Mei Mosi. Utumishi ilikabibidhiwa kombe hilo na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho Kikwete siku ya Mei Mosi, uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Watumishi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma wakisimama kwa dakika moja kumkumbuka mwenzao wa Ofisi ya Rais Ikulu aliyefariki ghafla wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi, Mei Day 2014 katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni